Saturday, 31 March 2018

Meneja Kampeni wa Mbunge Lema Ajiuzulu


Katibu Mwenezi wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo (kushoto).

Katibu Mwenezi wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia alikuwa Meneja Kampeni wa Mbunge wa Ausha Mjini, Godbless Lema, Gabrieli Kivuyo jana alikihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu ndani ya CHADEMA.
Aidha, amedai kuwa viongozi wake ikiwemo Mbunge kuwadharau pamoja na kitendo cha kutolewa nje kwenye kikao cha Mameya kwa tuhuma za kuwarekodi.

Akizungumza wakati akipokelewa na Katibu wa CCM-Wilaya, Musa Matotoka, amesema hata akipata matatizo na kumtafuta Mbunge amekuwa hapatiwi ushirikiano.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: