Mbunge Kingu ageuka 'mbogo' kwa wanaomjadili


Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi. Elibariki Kingu amefunguka kwamba yeye anakula bata (kufanya starehe) lakini pia anakumbuka kufanya maendeleo kwa kutumia uwezo wake binafsi ikiwa ni pamoja na 
wanachi na serikali kwenye jimbo lake.

Mh. Kingu amesema amesema maeneno hayo huku ikidhaniwa kwamba anarusha dongo kwa mtu anayemsema kwamba hafanyi kazi ambapo Mbunge huyo amesema kwamba "Najenga mashule mapya karibu kila eneo kwa nguvu zangu, serikali yangu na wananchi, nanunua vifaa Tiba na kuipa serikali zahanati zote kwa pesa ambayo walipaswa watumie wanangu".
Mbunge huyo amefafanua kupitia Mtandao wake wa Instagram kwa kuweka majengo ya kituo cha afya cha Ihanja ambapo amesema kuwa licha ya kituo hicho kuwa cha kisasa lakini pia kitakuwa na uwezo wakufanya mpaka upasuaji mkubwa.
Kituo cha Afya cha Ihanja kinachojengwa chini ya uongozi wa Mbunge Kingu
"Mjinga mmoja anakaa kwenye 'keyboard' anasema eti mbunge ana kula bata bata nakula lakini ninajenga zahanati kila kijiji jimboni kwa pesa zangu, serikali na wananchi," ameandika Mh. Kingu.
Mh. Kingu ameongeza "Nimesaidia akina Mama mitaji pikipiki zaidi ya 50 mpaka sasa za milioni 90 nimegawa kwa vijana kwa hela yangu. huyu mpuuzi akitaka ajue mapenzi ya hawa wananchi aje aongee huu upumbavu wake kwa wapiga kura wangu kama hawajamchoma moto".
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: