Friday, 16 March 2018

Mbowe atinga Kituo kikuu cha Polisi

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amewasili katika Kituo Kikuu cha Polisi leo Machi 16 saa 4:28 akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.

 Februari 20 mwaka huu, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliagiza kukamatwa kwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, akiwamo Mbowe.

Viongozi wengine waliotakiwa kuripotini Katibu Mkuu Vincent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika.

Wito wa kwenda polisi ulikuja siku chache baada ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji, (NIT) Akwilina Akwilin kuuawa kwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Kinondoni, Mkwajuni, jijini hapa.

 Akwilina alipigwa risasi hiyo wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: