Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikiria wanawake watatu kwa kutumia jina la Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na familia yeka kwa lengo la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Marchi 3 jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa Februari 23 mwaka huu kuliripotiwa kuwepo kwa watu wanaotumia jina la kiongozi huyo kushawishi watu kujipatia mkopo wa fedha kwa kujitangaza kwa kupitia ukurasa wake wa facebook uitwao, ‘Jakaya Kikwete Focus Vicoba’ na ‘Ridhiwan Kikwete Focus Vicoba’

Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao ni Mase Uledi(41) mkazi wa Kitunda, Khadija Khamis(42),mkazi wa Tabata na Mwange Uled(33) mkazi wa mkoa wa Bukoba. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na simu za mkononi 12 zikiwa na line za mitandao mbalimbali na huku wakiwa na line 10 zisizo kuwa ndani ya simu mabazo huzitumia ili kufanikisha uhalifu huo.

Watuhumiwa hao walifungua ukurasa ukurasa huo wa facebook na wamekuwa wakitumia line hizo za simu kuwapigia na kuwatumia meseji wananchi ili kuwashawishi kujiunga kwenye taasisi hizo na kisha kuzitumia line hizo kupokea miamala ya fedha kutoka kwa wakopaji wanaoshawishika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: