Masharti 10 ya kununua tiketi ya mechi ya marudiano kati ya Al-Masry na Simba SC

Tiketi za mechi ya marudiano kati ya waarabu klabu ya Al-Masry na klabu ya Simba zimeanza kuuzwa lakini masharti 10 muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata tiketi yako.
Tiketi hizo zimeanza kuuzwa mtandaoni na wanaohitaji wanatakiwa kujiandikisha kwa kufuata masharti 10 muhimu la sivyo huwezi kupata tiketi kwa namna nyingine.
Masharti au vigezo hivyo ni kujaza tarehe yako ya kuzaliwa na mwaka, Utaifa, kazi yako unayofanya, Eneo la makazi yako au sehemu unayoishi, Kuorodhesha majirani zako kwenye taarifa zako, Anuani yako au barua pepe, Namba zako za simu, Passport size, Namba ya kitambulisho cha uraia kwa wale ambao wana miaka kuanzia 18, lakini walio chini ya miaka 16 wataingiza taarifa kama hizo pamoja na vyeti vya kuzaliwa.
Kwa kufuata masharti hayo utakuwa umemaliza kujaza fomu na utasubiri majibu ya maombi yako kama utakuwa umekubaliwa au laa!
Ingia kwenye link ifuatayo (ticketing.3segypt.com) kununua tiketi yako au tembelea kwenye website ya klabu ya Al-Masry upate maelezo zaidi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: