Tokeo la picha la manara Yanga
Haji Manara


Msemaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara ameeleza kwanini klabu za hapa nyumbani hususani Simba na Yanga zinapocheza mechi za kimataifa zinaharibu nyumbani lakini ugenini zinacheza vizuri.
Manara amesema sababu kubwa ni kukosa UZALENDO kwa mashabiki wa timu zote ndio sababu inayopelekea klabu za nyumbani kuharibu michezo yao kwani mashabiki wanawafanya wachezaji wacheze wakiwa  na mashaka.
“Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo ya timu za bongo kutofanya vizuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo kwa vilabu vyetu. Wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na nikabezwa na viongozi wao..leo ndio mwaujua uzalendo?”ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, Manara amesema kwa sasa mashabiki wa Simba SC wataendelea kuwa wazalendo kwa timu ya taifa tu “Nawaambia kwa sasa tutafanya zaid yenu..kama tudini tudani….uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa tu
Jana klabu za Simba na Yanga ziliambulia sare ya bila kufungana dhidi ya vilabu vya Al-Masry na Township Rollers na kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa barani Afrika.
Mapema mwezi Februari Haji Manara aliwataka mashabiki wa klabu ya Simba kuwashangilia Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa dhidi ya Township Rollers.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: