Vinara wa ligi kuu soka nchini England Manchester City kupitia kwa Mkurugenzi wake wa michezo Ferran Soriano, imeweka wazi kuwa hakuna uwezekano wa kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Hakuna uwezekano wa kumsaini Messi, najua yeye na familia yake wanaishi vizuri na wanafurahia kuwa jijini Barcelona sehemu ambayo Messi anahitaji kuwa muda wote'', amesema Soriano.
Soriano ameongeza kuwa Messi amesaini mkataba mpya hivi karibuni na anaipenda klabu ya Barcelona kwani yeye binafsi anafahamiana vizuri na Messi hivyo anajua si Man City tu bali hakuna klabu ya kumtoa Messi ndani ya Barcelona.
Nyota huyo wa Argentina, mwezi Novemba mwaka 2017 alisaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Camp Nou hadi 2021. Mkataba huo unajumuisha kifungu cha timu inayomuhitaji italazimika kutoa kiasi cha Euro milioni 700 zaidi ya Trioni moja.
Messi leo atakuwa dimbani kuiongoza timu yake ya Barcelona kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea. Mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: