Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Aslay

Baada ya Rayvanny na Dogo Janja katika Music Facts leo tungependa kukufahamisha machache kuhusu Aslay.

Kupitia Music Facts ya Bongo5 tunakusongezea mambo 8 ya kawaida kabisa kuhusu Aslay ambayo ni kawaida kabisa na pengine si rahisi kuyabaini.
  1. Tangu Aslay kuondoka Yamoto Band amemshirikisha msanii mmoja tu katika nyimbo zake, naye ni Khadija Kopa katika wimbo uitwao Usitie Doa.
  2. Wimbo mrefu zaidi wa Aslay ni Likizo, wimbo huu una dakika 4:29, pia wimbo mfupi zaidi ni Baby ambao una dakika 3:09.
  3. Kwa kipindi cha takribani miezi 11 iliyopita (Apr 10, 2017-Feb 22, 2018) Aslay ametoa nyimbo zipatazo 15, sawa na wastani wa wimbo mmoja kila mwezi.
  4. Nandy ameimba maneno mengi zaidi ya Aslay katika wimbo Subalkher, Nandy ameimba maneno yapatayo 110 wakati Aslay ameimba maneno 108, ikiwa ni tofauti ya maneno mawili.
  5. Twitter ndio mtandao ambao Aslay ana followers wachache zaidi ukifuatia na facebook, katika twitter ana followers 2K na Facebook 49K, Instagram ndio anaongoza kwa kuwa followers Milioni 1.6.
  6. Wimbo wa kwanza wa kundi la Yamoto Band ulijulikana kwa jina la Yamoto, verse ya kwanza aliimba Aslay ila katika wimbo wa mwisho wa kundi hilo ‘Su’, verse ya kwanza aliimba Beka Flavour na Aslay alikuwa wa msanii wa tatu kuimba kutoka Yamoto Band baada ya Ruby ambaye walimshirikisha.
  7. Licha ya kutoa ngoma mbili pamoja ‘Subalkher na Mahabuba’, Aslay hajawahi kumshiriki Nandy katika wimbo wake wowote wala Nandy hajawahi kufanya hivyo, kilichofanyika wameshirikiana tu.
  8. Wimbo wa Aslay unaongozwa kwa kutazamwa zaidi katika mtandao wa YouTube ni Natamba. Wimbo huu ulitoka October 4, 2017 na hadi sasa una views 5.5 YouTube.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: