Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku kukamatwa wasanii pindi wanapokuwa wanapiga picha au kuigiza katika maeneo ya bandari yanayoonesha taswira ya Jiji inavyoonekana kiujumla kwa madai kitendo hicho wanalitalitangaza kitalii.
Makonda ametoa kauli hiyo leo (Machi 17, 2018) wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amepata malalamiko mengi kuhusiana na wasanii wanaokamatwa na wakiwa wapo katika shughuli za kuutangaza kiutalii mkoa wake.
"Kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam nimepewa taarifa kwamba kuna wasanii wakitaka kupiga picha katika baadhi ya kule kwenye meli 'bandarini' kwa kutaka kuonesha tu sura ya Dar es Salam inavyoonekana wakati wakitokea upande wa pili kule wa Kigamboni kuna watu wanajitokeza na kuwakamata wakati wanataka kuutangaza mkoa wao na vitu vizuri vilivyopo ndani yake", amesema Makonda. 
Aidha, Makonda amesema wasanii hao hao wakienda kuigiza katika maeneo machafu huwa hakuna mtu anayejitokeza kuwakamata au hata kuwazuia jambo ambalo lina mkera kwa upande wake.
"Sasa kuanzia leo hakuna kuwakamata wasanii wanapofanya matukio yao ya kurekodi ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wanakibali kutoka kwangu. Sehemu ambazo utahitaji kupata kibali ni Ikulu, Mahakamani na Jeshi la Polisi lakini hayo maeneo mengine yote unaruhusiwa kurekodi na huko wakitaka kibali njoo ofisini kwangu mimi nitakusaidia upate kufanya kazi yako", amesisitiza Makonda.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "leo hii Ikulu ya Marekani 'White House' inajulikana kutokana na muvi zao wengine hatujawahi kutembelea baadhi ya nchini lakini ukiangalia 'movie' unaambiwa ndio sehemu fulani unakubali kumbe hata wakati mwingine unadanganywa".
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema inapaswa ifike wakati wasanii waliopo nchini Tanzania hasa katika jiji lake wawe wanarekodi kazi za kwa uhuru bila ya kupatiwa shida ya aina yeyote ile.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: