Monday, 5 March 2018

Mabweni mawili Sekondari ya Wasichana Korogwe yateketea kwa Moto


MABWENI mawili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Moto huo ulianza kuunguza mabweni hayo saa tatu usiku na chanzo chake hakijajulikana.Hata hivyo inadaiwa huenda chanzo kikawa ni umeme ingawa bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa moto huo.


Akizungumza leo, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ,Edward Bukombe amesema atatoa taarifa rasmi na kwa sasa yupo eneo la tukio hilo."Nipo eneo la tukio na baada ya hapo nitakupa taarifa rasmi."
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: