Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali Leo wamekabidhi msaada wa Vitabu, Madaftari, kalamu na Matanki mawili ya kuhifadhia maji katika Shule ya Msingi Laibon iliyopo mkoani ARUSHA.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa hao- TAGCO, Pascal Shelutete amesema lengo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali za kutoa Elimu bure.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rashid Njarita ameshukuru kupokea msaada huo ambapo amesema matanki ya maji yataondoa changamoto ya maji iliyokuwepo shuleni hapo.

Msaada uliotolewa unathamani  ya shilingi milioni mbili na laki tano.

Maafisa hao wa Mawasiliano wanashiriki kikao kazi ambacho kinalenga kujengeana uwezo wa namna bora ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.

Kikao hicho kimeanza Machi 12 na kitamaliza Machi 16, 2018 huku kauli mbiu ya mkutano huo inasema Je ?Mawasiliano  ya kimkakati yanachagiza Vipi Tanzania ya Viwanda.

Imetolewa na;
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

15/3/2018

Share To:

msumbanews

Post A Comment: