Wednesday, 21 March 2018

KIJANA HUYU NI TUNU YA TAIFA- ACHAMBUA SEKTA BINAFSI NA TANZANIA YA VIWANDA.
Leo hii Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amekaa na kufanya mkutano na wawekezaji na wafanyabiashara wa Sekta binafsi.Katika mtazamo wa kiuchumi,Wachambuzi nguli Duniani wameeleza kuwa Baraza hilo la11 la wafanyabiasha na wawekezaji katika sekta binafsi ni ukweli usiopingika kuwa Serikali ya Tanzania inajaribu kwa namna yoyote kuthamini,kujali na kufungua milango na Mahusiano mazuri kati ya Serikali na Sekta binafsi toward National Economic Development (NED).

Ni ukweli usiopingika kwamba sekta binafsi ina mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote Duniani. Katika hali halisi hatuwezi kuzungumzia maendeleo ya viwanda, utatuzi wa tatizo la ajira na utoaji wa huduma bora za kijamii kama vile afya na elimu bila kutaja sekta binafsi.Sekta binafsi kwa tafsiri rahisi ni sehemu ya mfumo wa uchumi wa nchi ambayo inaendeshwa na watu na makampuni binafsi kwa lengo la kufanya biashara ili kutengeneza faida.

Sekta binafsi ni mifumo ya uzalishaji na ya kiuchumi ambayo haiendeshwi na Serikali.
Katika nchi yetu ya Tanzania tumeshuhudia ukuaji kwa kasi wa sekta binafsi na mchango mkubwa wa sekta hii katika kuchochea maendeleo ya Taifa letu.Kwa Mwaka 2015 -2020 inatarajiwa kutokea maendeleo makubwa na Mapinduzi ya Kiuchumi (Green Economy) Kupitia Sekta binafsi.

Sekta Binafsi imechangia kwa kiasi kikubwa katika  kutengeneza  ajira kwa vijana kwa kiasi kikubwa sana,Kwa maana Nyingine Sekta binafsi zinachukua nafasi Kubwa katika kuajiri na ndiye mwajiri mkubwa hapa nchini ikisaidiana na Serikali.Hivyo mchango wa Sekta binafsi ni kuntu katika Mataifa makubwa kama Marekani,China ,Uingereza nk.Mbali na mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuajiri nguvu kazi ya Tanzania, sekta hii ndiyo yenye mchango mkubwa katika kuongeza mapato ya serikali kwa njia ya kulipa kodi.

Aidha tangu nchi yetu iingie kwenye mfumo wa soko huria na ubinafsishaji wa mashirika ya umma, sekta binafsi imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi. Kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hasa za walaji (Consumers) umechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi hivyo kulinda thamani ya shilingi (Currency value) yetu na kupunguza kasi ya mfumuko wa bei (Inflation).

Sekta binafsi inachangia pia maendeleo ya nchi yetu kwa kuingiza teknolojia (Technological Transfer) mpya hapa nchini na pia inazalisha bidhaa mpya (New Brand) zenye ubora zaidi, imesaidia kuingiza mitambo ya kisasa katika kuchochea uzalishaji viwandani na kufanya kuwa rahisi,wa haraka na Bora Zaidi.Sekta binafsi ndiyo imekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa sekta ya kilimo (Agricultural Industries) na viwanda hapa nchini.Ukuaji wa sekta ya mawasiliano hapa nchini umechangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali Makini ya Mh.Rais (JPM) ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM). Hivi sasa hapa nchini suala la mawasiliano ya simu si tatizo tena kwa wananchi tofauti na ilivyokuwa miaka 10 au 15 iliyopita.Nakumbuka NYUMBANI kwetu Dodoma ulikuwa Lazima upande juu ya mti ili uwasiliane kwa miaka 10 iliyopita.Sasa unapiga simu mahala popote pale.Haya ni maendeleo makubwa kuwahi kufikiwa nchini.

Pamoja na mchango mkubwa wa sekta binafsi (Private Sectors) katika kuchochea maendeleo ya Taifa letu bado sekta hizi zimekutana na changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine ndizo zilizomfanya Mtukufu Rais wa Jamuhuri ya Muungano leo hii kusikiliza na kuongea na Wafanyabiashara katika sekta binafsi.Aidha lazima Serikali iweke mikakati maalumu ya kuzishughulikia changamoto zilizotolewa na Wafanyabiasha leo ili kasi ya maendeleo ya nchi yetu iwe kubwa zaidi.

Ikumbukwe katika kushughulikia na kutatua changamoto za sekta binafsi Kuna mambo ambayo ni dhahiri kuwa ni wajibu wa Serikali kuyashughulikia ili kuchochea ufanisi wa sekta hii na ukuaji wake kwa ujumla.Aidha Sekta binafsi na Serikali kuna (Win to Win Situation)Ambayo wafanyabiashara yamkini wanahitaji afueni ya Serikali ili watengeneze faida Zaidi na Serikali inaweka Sheria na Taratibu ili kudhibiti mapato ya Serikali.(Government Revenue).Kwa hiyo serikali inaposhughulika na kutatua changamoto za Sekta binafsi inahitaji kuwa Makini ili kuepuka hali ya  "Mwambangozi huvutia kwake".

Mh.Rais Dk. John Pombe Magufuli  amekuwa mstari wa MBELE na kuwahakikishia  Watanzania kuwa  rafiki mzuri wa sekta binafsi kwa masilahi ya Taifa letu,Na ndio maana Leo hii katika balaza la 11 la Sekta binafsi amedhihilisha nadhili yake.Sisi sote tunashuhudia utekelezaji wa ahadi zake kwa Watanzania wote kwa kasi ya ajabu sana. Ni jukumu letu kumwombea na kumpa ushirikiano mkubwa ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri zaidi ili kuliwezesha Taifa letu kupiga hatua za Haraka  kimaendeleo.

Aidha ili kuchochea maendeleo ya nchi Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara hapa nchini ili kuiwezesha Sekta binafsi kujiendesha kwa kufuata Kanuni,Sheria na Taratibu za nchi. Ni wajibu wa Serikali pia kuhakikisha kuwa tatizo sugu la upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika linaisha ili viwanda vyote hapa nchini viweze kuzalisha kwa ufanisi mkubwa.
Aidha ni muhimu sana sera, sheria na kanuni zote zinazohusu masuala yote ya sekta binafsi ziwe zinatekelezeka na zilenge katika kuchochea maendeleo ya sekta hiyo na Taifa kwa Ujumla.

Serikali ya awamu ya Tano ya CCM, imepunguza na kuondoa utitiri wa kodi na urasimu katika ulipaji wake ili kuwezesha Sekta binafsi ku-enjoy mazingira mazuri ya Biashara,Uwekezaji na  ukuaji wa sekta binafsi nchini.Serikali hii ya JPM imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara na reli (STANDARD GAUGE) ikiwa ni kichocheo kikubwa cha uwekezaji mijini na vijijini kwa kusafirisha malighafi na bidhaa za viwandani.
Kuna umuhimu pia kwa Serikali kuzuia utoaji wa vibali vya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi hasa kwa bidhaa ambazo zinazalishwa au zinaweza kuzalishwa hapa hapa nchini. Utaratibu huu utasaidia kulinda viwanda vya ndani na soko lake pia.

Serikali nimejitahidi  kudhibiti mfumuko wa bei (Inflation)na kuondoa urasimu uliokuwepo katika ofisi za umma,Haya ni mambo muhimu sana katika kuchochea ustawi wa sekta binafsi hapa nchini.Pamoja na mambo mengine ni muhimu sana kuweka kipaumbele na upendeleo maalumu kwa wawekezaji wa ndani ili kuchochea ukuaji wao kiuchumi kwa masilahi ya Taifa letu.Motisha (Motivation) inahitajika kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo na nishati hapa nchini. Kuna umuhimu mkubwa wa kuweka upendeleo maalumu kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji kutokana na ukweli kwamba sekta ya kilimo imeajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wote.Uwekezaji katika viwanda na biashara ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na kilimo kutachochea kwa kiasi kikubwa mapinduzi ya sekta ya kilimo hapa nchini.

Nchi yetu imeweka mipango mbalimbali ya maendeleo ambayo ipo kwenye utekelezaji wake. Mipango hiyo ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, MKUKUTA II na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka Mitano 2015/2016 – 2020/2021. Mipango hiyo yote imelenga katika kuondoa umaskini na kuleta maisha bora kwa Watanzania wote. Mafanikio ya utekelezaji wa mipango hiyo inategemea kwa sehemu kubwa ushiriki na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kupanga, kutekeleza na kutathmini mafanikio ya utekelezaji wake.

Ili Serikali yetu iweze kutimiza wajibu wake kwa wadau wa sekta binafsi ni lazima kwa wanaohitaji haki hiyo watimize wajibu wao. Kuna mambo ambayo wadau wa sekta binafsi kwa ujumla wao ni lazima wayatimize kwa ustawi wao na ustawi wa nchi yetu. Suala zima la ulipaji wa kodi stahiki kwa serikali ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu.
Serikali ikiwa na mapato ya kutosha ndipo inakuwa na nguvu zaidi ya kugharimia miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa barabara, reli na miundombinu ya umeme mijini na vijijini ambayo pia itawafaidisha wadau wa sekta binafsi katika kuendesha shughuli zao.
Pamoja na ukweli kwamba sekta binafsi imeajiri asilimia kubwa ya waajiriwa wote nchini ni muhimu pia kuangalia suala zima la ujira wanaopata waajiriwa kutokana na kazi wanazofanya.

Ujira uendane na hali halisi ya maisha ya Mtanzania pia waajiri wazingatie sheria za kazi kwa wafanyakazi wao. Lakini pia kwa wale wenzetu ambao wameamua kuwekeza kwenye kutoa huduma kama vile elimu na afya, gharama za huduma hizo zisiwe kubwa kiasi cha kumuumiza Mtanzania mwenye kipato cha chini.Wakati umefika sasa kwa kila upande yaani sekta binafsi na sekta ya umma kutimiza wajibu wake ili kuchochea zaidi maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu

Asante ni sana.

Netho Ndilito
(Hard Working & God Fearing Servant)
19.03.2018
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: