Johari kugombea Ubunge 2020 kupitia CCM


Msanii wa Filamu Bongo, Johari ameweka wazi mipango yake ya kugombea Ubunge.
Akizungumza kupitia Kikaangoni, EATV amesema ana mpango wa kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi mwaka 2020 kupitia CCM.
“Nina mapenzi sana na Chama Changu (CCM) na nina mpango mwaka 2020 kugombea Ubunge, nia ninayo na uwezo ninao,” amesema Johari.
“Sihitaji kuviongelea hivyo vitu kwa sana, nitakapo kuwa tayari nitakuja kuviongelea zaidi,” ameongeza.
Hata hivyo ameongeza kuwa hapendi kuchanganya siasa na kazi yake ya uigizaji kwa sababu mashabiki ni wa kada mbalimbali za kisiasa na kufafanua kuwa anapokuwa kwenye siasa ni maisha yake binafsi na anajulikana kama Blandina ila anapokuwa kwenye uigizaji ndiye Johari.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: