Faiza Ally: Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto gerezani - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 22 March 2018

Faiza Ally: Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto gerezani

Faiza Ally na mwanaye.

MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni mzazi mwenza na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, Faiza Ally amefunguka kuhusu kumpelekea mtoto gerezani kumuona baba yake huyo alikofungwa kwa miezi mitano.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kumpeleka mwanaye akamuone baba yake gerezani Mbeya na kumjulia hali, Faiza alisema kuwa, hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Sugu siyo ndugu yake.

“Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli,” alisema Faiza.

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done