WAZIRI wa Mambo ya ndani, Dk.Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya za Serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Dk.Mwigulu ameyasema hayo jana katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.

Amesema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa Serikali kwani yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

"Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa," amesema Dk. Mwigulu.

Amesisitiza wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya Serikali bila kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.

"Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya bali kuwa na mitazamo chanya na ukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro," amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: