Aliyekuwa diwani wa Kata ya Olsunyai mkoani Arusha, Elirehema Nnko kwa tiketi ya (CHADEMA) ambaye amekihama chama chake na kujiunga CCM amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaangalia watu wa kuwachukua kutoka upinzani.
Elirehema Nnko amesema hayo alipokuwa akihojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa yeye amechukuliwa na CCM kwa kuwa anajiweza na kudai ili uchukuliwe na CCM basi lazima uwe jembe kwani kitu kizuri kinajiuza. 
"Sikiliza nikwambie CCM wenyewe wanaangalia mtu wa kumchukua hawachukui tu kila mtu lazima kidogo uwe unajiweza yaani uwe jembe na unaweza kupiga kazi wewe unafikiri kuna mtu anachukua mazaga zaga, mimi najua kizuri kinajiuza pia" 
Mbali na hilo Diwani huyo ameelezea kuhusu baadhi ya picha zake zenye utata na kusema kuwa watu ambao wanamzungumzia vibaya kuhusu mapozi yake hayo ni wana wivu na yeye hakuna lingine ila yeye amechukulia hilo kama ni mtu ambaye ana nguvu ndiyo maaana watu wanamzungumzia sana.
Viongozi wengi wa upinzani wanapohama kutoka vyama vyao na kwenda CCM wamekuwa wakisema kuwa wanavutiwa na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, wengine wakisema wanavutiwa na kasi ya Rais lakini huyu amedai ameenda kwaajili ya biashara zake.  
Share To:

msumbanews

Post A Comment: