Saturday, 24 March 2018

Diva: Natongozwa zaidi ya Mara 2000 kwa Meseji, Nalazimika Kubadili Laini hata Mara 7 kwa Mwezi


Mtangazaji maarufu wa kituo cha Clouds FM, Diva The Bawse amedai kuwa baada ya kumwagana na aliyekuwa Boyfriend wake Heri Muziki amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa wanaume hadi inakuwa kero.

Akifunguka kwenye mahojiano yake na Bongo5, Diva amesema kupitia simu yake ya mkononi amekuwa akipata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume wengi wakimtongoza, kitu ambacho kila mwezi kinamfanya abadilishe laini zake mara saba.

Maisha ya kuwa single ni mazuri ingawaje nimekuwa nikipata usumbufu mkubwa kwenye simu yangu yaani napata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kwani wananifanya nibadili laini mara saba kwa mwezi,“amesema Diva.

Mbali na usumbufu huo, Diva amesema kuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram pia amekuwa akikumbana na usumbufu kama huo DM.

Kwa sasa mrembo huyo amesema kuwa ameshapata mwanaume ambaye ndiye anaamini kuwa atakuwa baba watoto wake siku za usoni ingawaje amekataa kumuweka wazi kwa sasa.

Kwa upande mwingine Diva ametangaza kuachia albamu yake mwaka huu ya ‘ALA ZA ROHO’ ambayo itakuwa na mastaa kibao kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a comment