BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi watano wapewa masharti ya dhamana


Leo March 29, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kwa kuwa na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini Bondi ya Shilingi Milioni 20.

Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho, ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Central Police mara moja kwa wiki.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa wataka rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kwa Mbowe na wenzake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: