Bocco ashindwa kujiunga na Taifa Stars

Nahodha wa Simba, John Bocco ameshindwa kwenda kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa nchini Algeria.

Bocco ambaye aliitumikia Simba dhidi ya Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho ameshindwa kwenda kutokana na kutokuwa fiti.

Baada ya mechi ya jana, Bocco ameonekana kuwa na maumivu hivyo tayari ameanza matibabu chini ya daktari wa Simba.

Wachezaji wengine watano wataondoka leo kwenda Algeria kuungana na Taifa Stars itakayocheza mechi ya kirafiki.

Wachezaji hao watano ni Erasto Nyoni, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe na Aishi Manula.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: