Zikiwa zimesalia takriban siku tatu kabla ya kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC haikijavaana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) utakaofanyika uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameiyambia tovuti  ya timu hiyo kuwa mchezo huo ni muhimu kwao na ndiyo nafasi pekee ya dhahabu waliyonayo itakayo wahakikishia kushiriki michuano ya kimataifa kwa upande wa kombe la Shirikisho.
Mchezo huu ni muhimu sana kwetu mshindi atasogea mbele zaidi kwenye nusu fainali na ukichukua kombe utapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, na sisi ni nafasi pekee ambayo kwetu sisi tunaiona ni nafasi ya dhahabu kuigombea hii ili kutimiza malengo yetu.
Timu hizi tayari msimu huu zimeshakutana marambili kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara na kutoka sare ya mabao.
Hizi ni rekodi za timu hizi kwa mechi sita walizocheza hivi karibuni kwa mashindano yote.
Azam FC imeshinda mechi nne kati ya sita na kutoka sare mbili, ilishinda mfululizo dhidi ya KMC (3-1) ukiwa ni mchezo hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, ikazifunga Singida United (1-0), Mwadui (1-0) na Mbao (2-1), lakini katika mechi mbili za awali ilitoka sare ugenini ilipocheza na Kagera Sugar (1-1) na Lipuli (0-0), zote zikiwa za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Kwa upande wa Mtibwa Sugar kwenye mechi sita zilizopita imeshinda mechi mbili dhidi ya Dodoma FC ikishinda 2 – 1 na ilipo ifunga Buseresere mabao 3-0 kwenye hatua ya 16 bora ya ASFC, huku katika mechi nne za ligi zilizobakia ikifungwa mara nne ilipokipiga na Stand United (2-1), Mtibwa Sugar (3-1), Ruvu Shooting (2-1), Tanzania Prisons (2-1).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: