Sunday, 11 March 2018

Aslay ampiga marufuku mama mtoto wake


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa ni gumzo kwenye mitaa ya bongo Aslay, amefunguka kuhusu kumpiga marufuku mama mtoto wake, kufanya kazi aliyokuwa akiifanya.
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Aslay amesema mama mtoto wake ambaye anafahamika kwa jina la Tessy, hawezi akaendelea kufanya kazi ya aliyokuwa akifanya ya 'video vixen', kwani amempiga marufu na kila alichokuwa akitafuta anampatia.
“Hawezi kuendelea mimi ndio nimesema hawezi kuendelea, sidhani kama sasa hivi anapenda tena kufanya, kwa sababu mara nyingi yupo na mtoto, na yeye  mwenyewe kuna mambo yake anafanya kitu kinachomuingizia hela, kwa sababu kule alikuwa anatafuta hela sasa hivi hela anapata”, amesema Aslay.
Msanii huyo pia ameweka wazi kuhusu tetesi za kuachana na mama mtoto wake huyo, na kusema kwamba hajawahi kuachana wala kutengana naye.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: