Chama cha ACT Wazalendo kimekabidhi mifuko 40 ya Saruji Kama mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya kujenga Zahanati kwenye Kijiji cha Chidolu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma ambacho kinaongozwa na ACT Wazalendo.

Wanachama wa ACT Wazalendo wakiwa katika picha ya pamoja
Ahadi ya kujenga zahanati hiyo ilitolewa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe. Akizungumza Wakati wa kukabidhi mifuko hiyo ya Saruji, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alisema yupo kumuwakilisha Kiongozi wao wa chama.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu akisaidia kubeba Cementi walizozitoa.
“Nipo hapa kumuwakilisha Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe ambaye aliahidi kushirikiana na nyinyi kuhakikisha Kijiji hiki ambacho kinaongozwa na ACT Wazalendo kinapata Zahanati ya Kijiji. Yeye yupo kwenye ziara ya kuzitembelea Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo. Sisi ACT Wazalendo tunaamini kwa dhati kuwa mbali na kutekeleza wajibu wa kuikosoa serikali, tunao pia wajibu wa kushirikiana na wananchi katika kujiletea maendeleo. Kazi ya upinzani haiwezi kuwa kupiga mdomo pekee. Itakuwa ni faraja iwapo Kijiji hiki ambacho hakina Zahanati tangu uhuru kitapata Zahanati katika Uongozi wa ACT Wazalendo,” alisema Ado.
Ndugu Ado aliwapongeza wananchi wa Chidolu kwa kujitolea kuchimba msingi wa Zahanati na kufyatua matofali.
“Maendeleo ya Kweli hayawezi kushushwa kutoka juu. Wananchi ni lazima washiriki kikamilifu kwenye programu za maendeleo. ACT Wazalendo tutaendelea kutoa mchango wetu Ili kutekeleza ahadi ya kujenga Zahanati hii. Lakini ni muhimu wananchi mshiriki kikamilifu hasa katika kujitolea nguvu kazi.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: