Sunday, 25 March 2018

Abiria Wakwama Nje kidogo ya Jiji la Arusha


Gari la ILYANA linalofanya safari zake kutoka Arusha kuelekea mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya limeharibika asubuhi ya leo na kusababisha abiria kukwama kwa zaidi ya saa 6 baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuharibika kila mita chache baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi mkoani Arusha.

mmoja wa abiria wa gari hilo amesema kuwa mpaka sasa hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo wala  gari lingine la kuwawezesha kuendelea na safari yao,hivyo ameomba vyombo vya ulinzi na usalama barabarani wajaribu kufuatilia chanzo cha tatizo hilo na kuwasaidia abiria kuweza kusafiri salama na kuendelea na shughuli zao nyingine.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: