Mbunge Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amemtembelea Tundu Lissu nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu ya viungo na saikolojia tangu Januari 7, 2018.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki anapata matibabu hayo baada ya kushambuliwa kwa risasi  Septemba 7, 2017 akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma. 

Awali mbunge huyo alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Dodoma siku hiyohiyo kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi alikotobiwa hadi Januari 6, 2018 alipohamishiwa Ubelgiji.

Katika picha mbalimbali zilizotoka jana Februari 11, 2018  ziliwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye mwonekano tofauti wa mazungumzo.

Leo Februari 12, 2018, Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS) amesema, “Zitto amekuja kunijulia hali na kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu hali ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii.”

Hata hivyo, Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo amesema hawezi kuzungumza zaidi kuhusu kile walichoteta na Lissu huku akiahidi baadaye kutoa taarifa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: