Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto Zuberi amechukuliwa maelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, Polisi wanaituhumu ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali katika mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.

Hivyo, ndugu Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Lakini kosa hilo amefunguliwa peke yake tu.

Baada ya kuandika maelezo akiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula, tokea saa Saa 4:42 usiku wa jana, mpaka saa 5:40 usiku, Jeshi la Polisi wamekataa kumpa DHAMANA kwa maelezo wanasubiri maelekezo toka kwa wakubwa wao. Hivyo ndugu Zitto amewekwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.

Pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti yake ni yapi, na wamekataa  pia kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria au la.

Emmanuel Lazarus Mvula
Wakili wa ndugu Zitto
Morogoro
Februari 23, 2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: