Yalojiri kwenye Mkutano wa Baraza la madiwani la robo ya pili 2017/18

Idara ya Ardhi imetakiwa kuweka vibao vinavyotambulisha maeneo ya Halmashauri ya Arusha kwenye maeneo yote ya mipaka halmashauri.

Maeneo yote yanayomilikiwa na halmashauri ambayo hayajaendelezwa yakabidhiwe kwenye shule za jirani na maeneo hayo yatumiwe na shule hizo kama mashamba darasa na baadaye shule hizo kujipatia chakula cha wanafunzi kwa muda wote ambao halmashauri inasubiri utekelezaji wa mipango iliyokusudiwa katika maeneo hayo.
Watumishi wa serikali wametakiwa kuacha tabia ya kujihusisha na masuala ya siasa kwenye maeneo yao ya kazi badala yake kufanyakazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia sheria na kanunu za utumishi wa Umma na kuwahudumia wananchi bila kujali itikadi zao kwa maslahi ya taifa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kujitoa kuchangia shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao kwa kukubaliana wenyewe kwenye mikutano ya vijiji hasa kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule za kutwa waweze kupata chakula cha mchana wawapo shuleni.
Wananchi wametakiwa kutambua umuhimu wa kulipa kodi na ushuru elekezi kwa kuwa mapato hayo ndio yanaendesha halmashauri ikiwemo miradi na shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwenye vijiji vyao kwa kurudishiwa asilimia sitini ya mapato hayo.
 Halmashauri bado inakabiliwa na changamoto ya nyumba za watumishi hasa wanaofanyakazi kwenye kata za pembezoni maeneo ambayo hakuna nyumba za kupangisha jambo linaloathiri utendaji wao wa kazi.
Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni imetakiwa kuweka mikakati thabiti ya kupata eneo la kujenga ofisi za kudumu za Mamlaka hiyo.
 Ifahamike kuwa Kijiji cha Madebe kilichoko kwenye mpaka wa halmashauri ya Arusha na Meru kipo halmashauri ya Meru na si halmashauri ya Arusha, hii ni kwa mujibu wa GN no 190 ya mwaka 2007 inayogawa halmashauri ya Arusha na halmashauri ya Meru.
 Madiwani wametakiwa kufanya mikutano ya kata 'WDC' kwenye kata zao pamoja na kukutana na wananchi kwenye Mikutano mikuu ya vijiji na kuwaelezea shughuli za maendeleo zinazotekelezwa kwenye maeneo yao ikiwemo miradi inayotekelezwa huko pamoja na kusimamia usomaji wa taarifa za mapato na matumizi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: