Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ametoa onyo kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora wanaoendeleza ujenzi na kilimo kwenye hifadhi ya barabara ilihali serikali imetumia fedha nyingi kulipa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.

Prof. Mbarawa amesema serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 894 kutekelza miradi mikubwa minne ya barabara wa kiwango cha lami zenye urefu wa zaidi ya kilomita 500 Mkoani Tabora.
"Miundombinu ya barabara ndio kiungo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote hivyo wananchi mnapswa kuwa walinzi wa utunzaji wa barabara hizo", amesema Prof. Mbarawa.
Kwa upande mwingine, Waziri huyo wa Ujenzi amesema wakazi wote ambao watakua wameingia katika maeneo ya barabara hawatalipwa fidia yoyote na kuwataka waondoke haraka huku akisema serikali haitasita kuwalipa wale wote watakaopisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa sheria.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: