WAZIRI WA ELIMU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA AKWILINA AKWILINE


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa  Joyce Ndalichako leo ameongoza Wananchi mbalimbali kuaga mwili wa aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) marehemu Akwilina Akwiline jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kumuaga Marehemu Akwilina Waziri Ndalichako amesema msiba huo umemgusa kila Mtanzania kwa kuwa Marehemu amekutwa na umauti akiwa anatekeleza majukumu yake ya kielimu.

Aidha, Waziri Ndalichako amezitaka Mamlaka zinazohusika kuharakisha kufanya uchungizi ili wale wote watakaobainika kuhusuika na tukio hilo waweze kuchukuliwa hatua  kwa mujibu wa  sheria za nchi.

Viongozi wengine walioshiriki kuaga mwili wa Mwanafunzi huyo ni pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad  Yussuf Massauni, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye , Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar e salaam Lazaro Mambosasa  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo.
Mwili wa Akwilina Akwiline tayari umesafairishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro na mazishi yanatarajiwa 0kufanyika kesho mkoani humo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

22/2/2018
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: