Waziri Nchemba atoa neno kwa Askari Magereza nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amewataka askari Magereza nchini kulinda taratibu za Magereza, kutokana na taarifa za baadhi ya askari wa jeshi hilo kuwapa simu wafungwa kwa ajili ya mawasiliano.

Waziri Nchemba amesema hayo katika uzunduzi wa gereza la Wilaya ya Chato, Mkoani Geita, na kuwataka Askari magereza hao kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao.

"Zamani unaweza kudhania kwamba wanasalimia familia lakini si sasa. Leo unaweza kumpa simu mfungwa ukidhani anasalimia familia kumbe anapanga mpango wa kuja kuwateka hapo hapo, majira yamebadilika. Sasa kwa sababu sheria zipo tuzingatie maadili ya sheria hizo ili kuweza kuhakikisha tunadumisha usalama na maadili magerezani", amesema Mwigulu.

Katika hatua nyingine Waziri Nchemba, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kuwachukulia hatua waliohusika na kifo cha Mwanafunzi pamoja na matukio mengine ya mauaji yaliyotekelezwa hivi karibuni.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: