Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dr Mwigulu Nchemba leo amewatembelea wafanyabiashara ndogondogo katika soko kuu la wilaya ya iramba, madereva pikipiki na madreva wa daladala na makodakta waliopo stand kuu ya mabasi kiomboi kuchungua changomoto wanazokutana nazo katika utendaji wao wa kazi ili kuwasilisha katika balaza la madiwani.

Kwa upande wa madereva wa bodaboda Dr Mwigulu amewashauli waendeshe bodaboda zao kwa usalama kwa kuzingatia sheria za barabarani ilikuepusha ajali na kukamatwa mala kwa mala na askari polisi pale wanapo kosea.

Wafanyabiashara ndogondogo wa soko kuu la mji wa kiomboi wamemuomba mbunge wao kuwasaidia kupunguza kodi nyingi ambazo wanakutana nazo wakati wanafanya biashara katika soko hilo na ombi lao kupokelewa na Dr Mwigulu akisema atakaa nao kuona njia nzuri za kutatua changamoto zao.

Baraza la madiwani linatarajia kukutana na mchana wa leo ambapo changamoto mbalimbali alizozipokea Dr mwigulu ataziwakilisha kupata utatuzi.





Share To:

msumbanews

Post A Comment: