Wednesday, 21 February 2018

Waziri Mwigulu Apokea Tani 230 za cement kwa Ajili ya ujenzi nyumba za PolisiWaziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Dr Mwigulu Nchemba amepokea tani 230 za cement kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi pemba na tani 130 kwa ajili ya ujenzi wa hospital na mabweni ya wanafunzi katika jimbo la iramba kutoka kiwanda cha simba cement cha jijini Tanga

Waziri Nchemba amewashukuru kiwanda cha simba kwa kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii hasa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba bora za askari polisi na ujenzi wa hospital na mabweni na  kusema kuwa ni mfano wa kuigwa nchini

Dr Mwigulu ameyasema hayo leo jijini tanga katika kiwanda cha simba cement na  kuwataka watanzania na wafanyabiashara wenye uwezo kuchangia shughuli za maendeleo nchini kama kujenga vituo vya polisi, nyumba za askari polisi,magereza na zimamoto ili kuwapa morali ya kazi zaidi vijana wanaofanyakazi masaa 24 kulinda raia na mali zao.

"Mimi kama waziri nawashukuru sana simba cement kwa kuisaidia wizara yetu zaidi ya mifuko 5500 kwa ajili ya kusaidia polisi pemba ujenzi wa nyumba za askari ambao wanaishi katika mazingira magumu sana rai yangu kwa watu wenye uwezo tunawakaribisha" alisema Dr Mwigulu

Naye Mwenyekiti wa Halamsauri ya wilaya ya Iramba Saimon Mkumbo Tyosela amemshukuru mbunge wa jimbo la iramba Dr Mwigulu Nchemba kusaidia kufanikisha kupatikana kwa cement ambazo zitatumika ujenzi ambao ulisimama kutokana na kukosekana kwa fedha za kuendeleza ujenzi huo na kusema sasa tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike katika wilaya ya iramba linakwenda kupungua kama si kuisha kabisa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Simba cement mhandisi Reinhardt Swart amesema wawao kama kampuni huwa wanasaidia sana shule zikizo katika mkoa wa tanga lakini sasa wameamaua kusaidia taasisi zingine za serikali amabazo zinauitaji wa kuboresha miundombinu kama wanavyofanya kwa polisi pemba na shule na hospital za Iramba.

Waziri Dr Mwigulu alipata fursa ya kutembeza maeneo mbalimbali ya kiwanda cha simba cement kuangali jinsi wanavyochimba malighafi mpaka uzalishaji wa cement unavyofanyika kiwandani hapo ambacho kimeajili watanzania 300 na vibarua 3000.Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: