Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Daniel John ambaye alikiwa ni katibu wa Chadema kata ya hananasif  yaliyotokea kinondoni  jijini Dar es salaam.

Waziri Dr Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

"Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili". Alisema Waziri Mwigulu

Ameongeza kusema kuwa maswala ya demkrasia huamukiwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: