Waziri Kigwangalla aahidi kutoa ushahidi bungeni dhidi ya Mch. MsigwaDkt. Hamisi Kigwangalla

Baada ya Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA) Mhe. Mchungaji Peter Msigwa kumshambulia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kudai kuwa ameshindwa kutoa ushahidi bungeni juu yake kuhusu ufisadi kwenye vitalu na kuja mtandaoni kuanza kulalamika. Hatimaye Mhe. Kigwangalla ametangaza kuanika ushahidi wote bungeni

Waziri Kigwangalla amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amemjibu Mchungaji Msingwa kuhusu ushahidi huo kwa kumwambia kuwa tayari anauandaa  na atauwasilisha bungeni kwenye vikao vinavyokuja.

Unataka nitoe ushahidi bungeni? Really? Haya subiri. Ngoja nihamishie kwenye flash kisha nitaweka mezani bungeni one of these days!“ameandika Kigwangalla.

Awali Waziri Kigwangalla akiwa bungeni kwenye vikao vya Bunge lililopita alidai kuwa ana taarifa za maslahi binafsi ya Mbunge Peter Msigwa kuhusu vitalu na kudai kama angelisema hilo bungeni anaamini bunge lingechafuka hivyo aliamua kukaa kimya na kutulia ili kuepusha ugomvi na mtu binafsi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: