Waziri wa Afya nchini Zimbabwe David Parirenyatwa ameyataka makampuni yanayoingiza condom nchini humo kuzingatia ubora na vigezo, kwani condom nyingi wanazoingiza zinakuwa hazina viwango na ubora, huku wengi wakilalamikia kutowatosha.
Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya sekta binafsi inayoshughulika na masuala ya HIV na UKIMWI, na kusema kwamba condom nyingi huwa zinaingizwa kutoka China, na zimekuwa zikilalamikiwa kutowatosha wananchi wanaozitumia.
“Mnajua kuwa ukanda huu wa Kusini mwa Afrika kuna maambukizi makubwa, na tunahamsisha kutumia condom kwa wote wake na waume, vijana siku hzi wana condom zao wanazopenda lakini hatuzitengenezi hapa, tunaingiza condom kutoka China, wanaume wengi wanalalamikia kuwa ni ndogo sana. Tunatakiwa tuliangalie hilo, mnatakiwa muweze kuwa na condom zenu wenyewe, kama mnataka kuwa wafanya biashara wakubwa, hivyo mzizalishe hapa hapa”, amesema Waziri huyo.
Matumizi ya condom nchini humo yametajwa kuwa ni makubwa nchini humo, ambapo mwaka 2016 zaidi ya condom milioni 109 ziligawiwa kwa wanaume, ambazo ni sawa na condom 33 kwa kila mmoja kwa wastani, na kuifanya nchi hiyo kufikia viwango vya UNDP.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: