Baadhi ya waombolezaji ambao walijitokeza kuaga mwili wa marehemu Akwilina aliekua anasoma katika Chuo Cha Usafirishaji (NIT ) jijini Dar es Salaam wamepokonywa mabango mbalimbali ambayo yalikuwa na jumbe mbalimbali kuhusiana na kifo hicho. 

Waombolezaji hao ambao wengine walikuwa wameshika mabango kuhoji uhalali wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Sirro kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa licha ya mauaji hayo kutokea.

Walijitokeza vijana mbalimbali ambao walikuwa wamevaa suti nyeusi na kuanza kupokonya mabango hayo kwa waombolezaji hao na kuondoka nayo, tukio hilo limetokea wakati Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako akihutubia mamia ya waombolezaji katika Viwanja vya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: