Wananchi wa kijiji cha Mkono wa mara Kata ya Mkambarani Wilaya na mkoa wa Morogoro, kwa pamoja wameazimia kusitishwa kwa shughuli zote za kiserikali ngazi ya kijiji hicho, ikiwemo ukusanyaji wa kodi mbalimbali.

Wanakijiji hao wamefikia maamuzi hayo wakati wa mkutano baina yao na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, uliolenga kujadili sintofahamu iliyojitokeza baada ya mkutano wa kijiji wa Disemba 27 mwaka jana ambao uliwavua mamlaka viongozi wa serikali ya kijiji.

Baada ya kutangaza kutokuwa na imani na viongozi wao,  Disemba 27, walichagua Mwenyekiti wa muda lakini maamuzi hayo yalipingwa na Viongozi wa Chama kuwa hayakufuata taratibu na kusababisha kukosa huduma kwa kipindi chote.

Aidha wananchi wamewaomba viongozi wa Chama hicho ngazi ya Kata na Wilaya kusitisha shughuli za kukusanya kodi hadi hapo watakapofanya uchaguzi na kupata viongozi wengine, kwani kwasasa hawana viongozi wa kusimamia shughuli hizo.

Kwa upande wa viongozi wa Chama ngazi ya kata na wilaya wameiomba serikali kufanya hima kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo kwani kuendelea kukaa bila uongozi kunakwamisha shughuli za maendeleo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: