IMG_20180226_163811
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno akizungumza alipotembelea kata ya Mapinga ,wilaya ya Bagamoyo wakati wa muendelezo wa ziara yake anayoendelea nayo mkoani hapo kushukuru kuchaguliwa nafasi hiyo.(picha na Mwamvua Mwinyi)
IMG-20180226-WA0008
Aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Mapinga kupitia ACT Wazalendo uchaguzi mkuu uliopita ,Tabia Juma akiongea baada ya kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno aliyoifanya wilayani Bagamoyo,pamoja na hilo uongozi mzima wa ACT kwenye kata hiyo ulihamia CCM.
IMG-20180226-WA0017
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani ,(hayupo pichani) wakati alipokuwa amefanya ziara yake ya kushukuru wilayani humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
Uongozi mzima wa Chama Cha Act Wazalendo Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani akiwemo aliyekuwa mgombea udiwani Tabia Juma ,wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao wameamua kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Ramadhani Maneno aliyoifanya Kata ya Mapinga,Bagamoyo.
Akiwapokea viongozi hao akiwemo Tabia, mwenyekiti Shaban Rashid na katibu mwenezi Omary Kibanda, Maneno alisema kwa sasa wapinzani hawana tena nafasi .
Alisema ,kutokana na ilani ya chama kutekelezwa vizuri na kuisimamia serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi kero nyingi zimepungua.
“Wapinzani wameshaona kwenye vyama vyao kwa sasa hakuna wanachokifanya zaidi ya kuwavuruga na kuwachanganya wananchi,” alielezea Maneno.
Alisema kuwa serikali inaendelea kutekeleza kwa vitendo yale yaliyoahidiwa lengo likiwa ni kuleta maendeleo.
Akizungumzia juu ya usimamizi wa miradi alisema chama kitaendelea kuisimamia serikali ili kuhakikisha miradi yote inakamilika.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, alhaj Abdul Sharifu alibainisha watahakikisha wanasimamia ilani ili utekelezaji wa miradi uwe na mafanikio.
Mwenyekiti huyo alisema , chama kimejipanga kuwatetea wananchi kwa kuondoa changamoto za maendeleo kwa kushirikiana na watendaji wa serikali.
Katika ziara hiyo , Maneno alitembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Kerege na kuzindua matawi ya chama .
February 27 ,ataendelea na ziara yake kwenye Jimbo la Chalinze kwa ajili ya kushukuru kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: