Kasi ya ulevi katika Wilaya ya Rombo imeelezwa kuwa imeanza kupungua baada ya serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo wilayani humo kutoa elimu juu ya adhari za ulevi kwa wanakijiji. Badhi ya wakazi wa Wilaya ya Rombo wakizungumza walisema kuwa wanaipongeza Serikali kwa kudhibiti ulevi saa za kazi kwani kabla ya kuwepo kwa sheria hiyo inayokataza kunywa au kuuza pombe muda wa kazi yani asubuhi hadi saa kumi jioni, watu wengi walikuwa wakitumia muda wao mwingi kukaa vilabuni badala ya kufanya kazi.
Aidha wameongeza kuwa ulevi unarudisha nyuma maendeleo na kupunguza nguvu kazi kutokana na vijana wengi kujiingiza katika ulevi na hivyo kushindwa kufanya kazi za maendeleo hali inayochangia umasikini katika jamii.
Mwenyekiti wa Kikundi cha umoja wa vijana wajasiriamali Juhudi Group, Venance Mushi alisema kuwa tatizo la ulevi limeanza kupungua katika wilya hiyo lakini pia ametoa ushauri kwa serikali kuendelea kutoa elimu zaidi ili tatizo hilo liweze kwisha kabisa kwani linaharibu sifa na taswira ya wilaya ya Rombo ambayo kwa sasa inasadikiwa kuwa ndiyo inayoongoza kuwa na ya kwanza kwa ulevi katika mkoa wa Kilimanjaro.
Wilaya hiyo ambayo ina viwanda vidogo vya pombe za kienyeji ambavyo vinakadiriwa kufika zaidi ya aina hamsini za pombe za kienyeji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: