Picha ya Maktaba




Ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 42.4 kutoka Ngaramtoni hadi Usa River inayotarajiwa kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Arusha unatarajia kugharimu Sh139 bilioni .
Ujenzi wa barabara hiyo utaanza Machi, 2018 na kukamilia Februari, 2019.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Arusha wametembelea barabara hiyo na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.
Akizungumza na wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo, Gambo amewataka kuwa wavumilivu na changamoto za sasa kwani kuanzia mwakani wataanza kufaidika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Dk Wilson Mahela amesema tayari wameanza kupokea kero wanazozipata wananchi kutokana na ujenzi huo na kuzipeleka kwa Wakala wa Barabara (Tanroads).
Meneja wa Tanroads Arusha, John Kalupale amesema ofisi yake ipo wazi kwa wananchi wenye kero kabla ya kuanza kuwekwa lami barabara hiyo.
"Tunapokea kero na ushauri lengo letu ni barabara hii kuwa na faida kwa wananchi na si kuleta matatizo,” amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: