Mkoa wa Dodoma una upungufu wa madarasa 6,643 ambayo ni sawa na asilimia 52 ya mahitaji yote ya madarasa mkoani humo.

Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo amesema, kwa sasa mkoa mzima unahitaji madarasa 12,664, wakati yaliyopo ni 6,056.

Amesema, wilaya inayoongoza kwa kuwa na upungufu mkubwa wa madarasa ni Bahi ambayo ina upungufu wa madarasa 988 sawa na asilimia 66.

Wilaya nyingine yenye upungufu mkubwa ni Kongwa ambayo ina upungufu wa madarasa 1,271 sawa na asilimia 64 ya mahitaji.

Chamwino ina upungufu wa madarasa 888 sawa na asilimia 53, Chemba ina upungufu wa vyumba 815 sawa na asilimia 54 na Dodoma Manispaa yenye upungufu wa madarasa 1,138 sawa na asilimia 57.

Wilaya ya Kondoa Vijijini ina upungufu madarasa 519 sawa na asilimia 45, Kondoa Mjini upungufu wake ni 185 sawa na asilimia 47 pamoja na Mpwapwa ina upungufu wa madarasa 839 sawa na asilimia 34.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: