Ubalozi wa China waunga mkono ujenzi wa ofisi za waalimu Dar - MSUMBA NEWS BLOG

Thursday, 15 February 2018

Ubalozi wa China waunga mkono ujenzi wa ofisi za waalimu Dar

Balozi wa china nchi Tanzania Wang Ke, Jumatano hii ameaahidi kujenga ofisi za walimu kila wilaya ya Mkoa huo ili kusaidia kuinua kiwango cha Elimu hapa nchini na kuunga mkono njuhudi za mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh.Ppaul Makonda.

Akizungumza katika uzinduzi huo Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, amesema nchi yake itaendelea kusaidia mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla katika shughuli za Maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi mpya za Walimu ili mpango wa elimu bure kwa watoto wa Tanzania uweze kufanikiwa.

“Ili Taifa liwe zero kuendelea ni lazima liwe na wataalam wa kutosha , hata sisi China tulia mualiko kuwekeza katika elimu na sasa angalau tuna ona tumepiga hatua kubwa nina imani nanyi kwa kushirikiana hasa ushirikiano na moyo aliounesha Mhe. Makonda mtafanikiwa” alisema Wang Ke.

Aidha Balozi huyo amepongeza uchapaji kazi wa Mhe. Paul Makonda na kumsifu akilinganisha na Mbwa kutokana na kuzaliwa mwezi huu kuwa nchi China ni mwezi wa mbwa na kufa fafanua kuwa watu walio zali wa mwezi huu ni wachapakazi kama alivyo Makonda
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda, amemshukuru Balozi wa China na kusema kuwa China ni rafiki wa kweli wa Tanzania kwa kuwa wamekuwa msaada mkubwa hasa katika shughuli za Maendeleo na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano kati shughuli zote za kiserikali katika mkoa wa Dar es Salaam.
“China imepiga hatua kubwa nataka Niwa ambie ninyi wanafunzi, wameniahidi kuwa Kuna Scholar ship za kwenda kusoma China na kujifunza kichina ni wakati sasa wa kujifunza kichina hili ndio Taifa kubwa kiuchumi hata Marekani wanakopa china na Wana daiwa”alisema
Amewataka wananchi wa Mkoa huo kuwapuuza viongozi wanaingia siasa katika ujenzi huo kwa kusema wa kikubali kujengwa ofisi za Walimu katika Wilaya zao kwamba Makonda atapata sifa.
Viongozi kama hao hawafai wanaturudisha nyuma kimataifa endeleo hawana nia njema na walimu wetu na watoto wetu.”Amesema
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done