Snura atoa siri nzito ya kibenten chake


Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Snura Mushi, amefunguka juu ya kijana anayeonekana naye mara kwa mara huku wengi wakiamini kuwa ni kiben ten chake, na kusema suala hilo halina ukweli.

Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Snura amesema tuhuma zinazomkabili kuhusu kijana huyu anayejulikana kwa jina la Minu Calypto, zimemfanya atoe siri ambayo hakutaka wajue, kuwa kijana huyo sio mpenzi wake bali amefanya naye video ambayo haijatoka, na ndipo zilipopigwa picha za mahaba zilisosambaa mtandaoni.
“Mimi na Minhal hatuna mahusiano, kisa picha!!? Picha ile ni video jamani hii sasa mnanilazimisha niseme siri  sasa, ni video ambayo haijatoka na imechelewa kutoka kwa sababu nimeimba na Aslay, na Aslay alikuwa na project yao ya Valentine, ndio maana amechelewa kuingiza vipande vyake ndio maana imechelewa kutoka”, amesema Snura.
Kijana huyo ambaye kwa sasa ameingia kwenye muziki wa bongo fleva, anatajwa kuwahi kutoka kimapenzi na msanii wa filamu bongo, Nisha bebe.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: