Thursday, 15 February 2018

Simba yakaziwa na Mwadui FC watoka sare

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba imekubali kutoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliyopigwa huko Kambarage Shinyanga.

Mabao ya Simba SC yakifungwa na John Bocco katika kipindi cha kwanza huku lapili likifungwa na Emmanuel Okwi kwa njia ya mkwaju wa penati wakati Mwadui wakipata mabao yao kupitia kwa David Luhende na Paul Nonga.

Kwa matokeo hayo Simba SC inafikisha jumla ya alama 41 ikiwa inaongoza msimamo wa ligi wakati Mwadui FC wakifanikiwa kufikisha jumla ya pointi 18.

Simba SC mchezo ujao wanatarajia kukutana na Mbao FC jijini Dar es salaam, Simba SC na Yanga SC mpaka sasa wanatofautiana kwa alama tano.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: