Klabu ya soka ya Simba jana imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikishinda kwa jumla ya mabao 5-0 na sasa itakutana na Al Masry ya Port Side Misri.

Simba inakumbuku nzuri katika ardhi ya Misri baada ya kufanikiwa kumtoa nje ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika aliyekuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo mwaka 2003 timu ya Zamalek.

Katika mchezo wa kwanza mabao ya Simba yalifungwa na Said Ndemla, John Bocco aliyefunga mawili na Emmanuel Okwi ambaye amefikisha mabao 16 ya kuifungia Simba msimu huu katika mashindano yote.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: