Sijawahi kutoka kimapenzi na TID, sio type yangu – Rachel


Msanii wa muziki Bongo, Rachel amesema hajawahi kutoka kimapenzi na TID kama inavyokuwa ikiripotiwa.
Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Same Boy’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hajawahi kubeba ujauzito wa TID.
“Niseme tu TID sio bwana yangu, sio mtu wangu, TID hawezi kuwa mtu wangu, TID mkubwa ujue, ana type zake, mimi nina type zangu za wanaume ambao natakiwa ni date nao, TID siyo type ya wanaume ambao naweza ku-date nao, kirafiki kuongea sawa,” amesema.
“Naomba nieleweke, sijawahi kutoka kimapenzi na TID, sijawahi kubeba mimba ya TID hata mara moja,” amesisitiza Rachel
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: