Ruvu Shooting hatujafa waulizeni Lipuli FC – Masau Bwire

Baada ya klabu ya Ruvu Shooting kuchomoza na ushindi mujarabu wa mabao 3 – 1 dhidi ya Lipuli FC msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire amesema kuwa kwa sasa lazima kuchomoza na pointi tatu kwa kila mchezo watakao cheza.
Bwire ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na kipindi cha michezo cha radio Magic FM.
“Hiyo ndiyo Ruvu Shooting mpira tunao cheza sasa timu yoyote lazima iwache pointi, ushindi huu tuliutarajia na tunakuja,”amesema msemaji wa Ruvu Masau Bwire.
“Sisi siyo watu ambao tuna kuja ila ni uwezo, Ruvu Shooting hatujafa, hatutakufa na wala hatutarajii kufa hebu waulize Lipuli FC tulicho mfanya.”
“Tunashukuru waamuzi walikuwa wazuri na wenye viwango vya hali ya juu vya kutafsiri kanuni za ligi kuu na hakuna waliyo walalamikia hata baada ya kumalizika kwa mchezo.”
Kufuatia matokeo hayo ya ushindi mnono wa mabao 3 – 1 dhidi ya Lipuli FC klabu hiyo ya Ruvu Shooting sasa inakuwa nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 20.
Michezo mingine iliyopigwa hapo jana na msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa sasa.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: