Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo ambaye jana alipata ajali baada ya gari lake kupasuka taili na kupinduka, bado anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Yusuph Ilembo amesema leo Februari 27 kuwa, Mkumbo amehamishiwa katika wodi maalumu baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Amesema hali ya Kamanda Mkumbo ambaye alijeruhiwa mkononi na kichwani kutokana na kupata michubuko ya vioo inaendelea vizuri.
"Hali ya kamanda inaendelea vizuri na bado anapatiwa matibabu na dereva wake," amesema.
Akizungumzia mpango wa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi, Ilembo alisema jambo hilo bado halijafikiwa uamuzi.
"Hospitali yetu ya mkoa ya Mount Meru bado haijashindwa kutoa huduma, hivyo bado ataendelea kuwa hapa," amesema
Kamanda Mkumbo alipata  ajali hiyo kati ya eneo la Mdori na Minjingu wilayani Babati majira ya saa nane mchana jana na alikuwa anatokea mkoani Singida kurejea Arusha.
"Gari lilipata ajali baada ya kupasuka taili la nyuma upande wa kushoto na kukosa mwelekeo 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: