Wednesday, 28 February 2018

Roma anavyovaa huwezi sema ni msanii – Madee

Msanii wa muziki Bongo, Madee amekosoa uvaaji wa msanii mwenzie, Roma.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Sema’ ameiambia Clouds TV avaaji wa Roma si kama wa msanii kitu ambacho amewahi kutaka kukirekebisha.
“Kati ya wasanii wa Bongo ambao wananiangusha kwenye kuvaa ni Roma nimewahi kufikiri siku nimpeleke dukani nikamfanyie shopping kwa maana anavyovaa huwezi sema ni msanii,” amesema Madee.
Kauli ya Madee inaweza kuchukuliwa ni kawaida kwa wasanii waliochini ya Tip Top Connection kwani kipindi cha nyuma Dogo Janja aliwahi kutoa kauli inayoshabiana na hiyo kwa kueleza hakuna msanii Bongo anayemfikia kwa kuvaa vizuri.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Madee na Roma ni wasanii ambao wamekuwa na utani wa hapa na pale ambao muda mwingine wanauingiza kwenye ngoma zao na hata kuhusisha ishu za kifamilia.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: