Friday, 16 February 2018

Ridhiwan Kikwete awaasa wakazi wa Kinondoni kuhusu Mtulia ‘tunachagua daraja’

Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa na Waziri wa Tamisemi ,Suleiman Jaffo
Mbunge wa Chalinze kupitia tiketi ya CCM, Ridhiwan Kikwete ni moja ya viongozi waliohudhuria kwenye kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni kumnadi Mgombea wa chama hicho, Maulid Mtulia na kuwaasa wananchi wa jimbo hilo kumchagua Maulid Mtulia
Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kinondoni wanapaswa kumchagua Mtulia kama kiongozi wao kwani yeye atakuwa daraja kati ya wananchi na Maendeleo.
Kinondoni tunachagua (Maulid Mtulia) Daraja litakayeunganisha wananchi na Maendeleo, #hapakazitu,”ameandika Mhe. Ridhiwan Kikwete kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Marudio ya Uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Februari 17, 2018.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: