Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo amepokea *shehena ya Makontena 20 Kati ya 36 yenye samani* (furniture) zenye thamani ya *Shillingi Billion 2* zilizotolewa na *Diaspora waishio Nchini Marekani* waliounga mkono kampeni ya *RC Makonda* ya ujenzi wa *Ofisi 402 za Walimu* Dar es salaam.

Ndani ya Kontena hizo zipo *Meza za umeme zenye hadhi ya kimataifa 2500, Meza za kawaida 2500,Viti zaidi ya 5,000,Makabati makubwa ya vitabu 1300, Ubao za kisasa (writing board) zisizotumia chaki 700* ambazo kwa kiasi kikubwa utaenda kupunguza *mateso ya walimu kuumwa vifua kutokana na vumbi la chaki.*

Vifaa hivyo vya kisasa vimetolewa na *Jumuiya ya watanzania waishio Marekani* ijulikanayo kama *Sixth Region Diaspora Caucus Washington* iliyomuunga mkono *RC Makonda* kutokana na kuguswa na kazi kubwa anayoifanya kwenye *kuboresha mazingira ya walimu.*

Akizungumza wakati wa kupokea makontena hayo *RC Makonda* amesema *jumla ya kontena zilizotolewa na jumuiya hiyo ni 36 na Kati ya hiyo 20 yamefika na mengine 16 yapo njiani* ambapo ameshukuru jumuiya kwa kutambua *thamani ya mwalimu.*

*RC Makonda* amesema lengo lake ni kuboresha mazingira ya walimu na kurejesha heshima yao ili  wapate *morali ya kufundisha* wanafunzi na mwisho wa siku kusaidia taifa kuwa na *wataalamu wa kutosha*.

Aidha ameshukuru *Bank ya Walimu* kwa kusaidia kulipia usafirishaji wa makontena matatu na kuwaomba *wadau kusaidia kulipia gharama za usafiri wa makontena mengine Kama mchango wa kutambua thamani ya mwalimu.*

Walimu walioshuhudia makontena hayo wamemshukuru *RC Makonda* kwa namna anavyoboresha mazingira yao ya kufanya kazi na kueleza kuwa *vifaa walivyovishuhudia* leo wanaamini sasa watafanya kazi kwa *bidii* zaidi na kuongeza *ufaulu* kwa walimu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: